Zelenskyy aomba msaada zaidi kuikabili Urusi, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    9,540 views
    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amehutubia viongozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kupitia video kutoka mjini Oslo, na kuomba washirika wake kutoa angalau euro bilioni tano ili kumuwezesha kupata makombora haraka iwezekanavyo. Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekutana kujadili changamoto za kiuchumi na kijeshi zinazolikabili bara hilo na pia jinsi ya kuimarisha uungwaji mkono kwa Ukraine.