Juhudi za kutafuta amani Sudan Kusini, katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    9,139 views
    Ujumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika umefika nchini Sudan Kusini kwa lengo la kufanya mazungumzo ya kuzuia kuzuka upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mpango huo unafuatia kuzuiliwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambaye ameshutumiwa na serikali ya Rais Salva Kiir kwa kujaribu kuchochea uasi-madai yanayohusishwa na mapigano ya hivi karibuni katika jimbo la Upper Nile. Mapema hii leo, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alikutana na Rais Kiir Juba. Maelezo mahususi ya majadiliano hayo hayajawekwa wazi, lakini yale yanayoendelea nchini Sudan Kusini yameibua wasiwasi kuhusu uthabiti wa mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw