Mawaziri wapya wapewa changamoto ya kumaliza jinamizi la ufisadi

  • | K24 Video
    6 views

    Baada ya kulishwa kiapo,mawaziri 19 wataanza kurekebisha sera na sheria ambazo zitakabiliana na ufisadi kikamilifu hasa katika taasisi za umma. Akiongoza hafla hiyo mapema asubuhi rais William Ruto amewataka mawaziri wapya kuweka maslahi ya wakenya mbele katika utendakazi wao, ili kuisaidia serikali kuafikia ajenda yake. Rais Ruto ameendelea kutetea hatua ya kujumuisha upinzani katika serikali yake ya Kenya Kwanza.