Mfahamu mvuvi mwanamke kutoka Kenya

  • | BBC Swahili
    73 views
    Pauline Mwaka Kalu ni mkaazi wa Kilifi katika eneo la pwani ya Kenya. Yeye anafanya kazi ya uvuvi baharini, kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na wanaume. Pauline sasa amewavutia wanawake wenzake kujiunga na taaluma hiyo licha ya kuwa katika baadhi ya tamaduni, ni mwiko kwa  mwanamke kujihusisha na uvuvi.