Mfanyikazi wa KQ Lydia Olando maloba anazuiliwa Jamhuri ya Congo

  • | Citizen TV
    1,624 views

    Familia ya mfanyikazi wa kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lydia Olando Maloba anayeendelea kuzuiliwa Jamuhuri ya Kidemokrasia Ya Congo sasa inataka jitihada zaidi, zaidi ya wiki mbili baada ya kuzuiliwa kwake. Familia yake ikiongozwa na mwanahabari mkongwe Leonard Mbotela ikisimulia jitihada za familia ambazo ziligonga mwamba licha ya jamaa na mawakili kufika nchinI DRC.