Mgogoro wa ngano Narok

  • | Citizen TV
    1,286 views

    Mgogoro wa uuzaji wa ngano nchini unaendelea kutokota. Ingawa tatizo hili limeripotiwa kuendelea kwa miezi kadhaa, mambo yalichukua mwelekeo tofauti wiki hii wakulima huko narok walipoandamana kupinga ukosefu wa soko la mazao yao. Kiini cha mgogoro huu ni madai kwamba wakulima wenye ushawishi mkubwa serikalini wamepanga njama ya kudhibiti ununuzi wa ngano. Hali hii inachangiwa pia na ngano inayoagizwa kutoka nje, matokeo yake ni maghala huko narok na maeneo mengine ya kilimo cha ngano yakijaa. Ben kirui alizuru maeneo mbalimbali ya kaunti ya narok na kuangazia hali halisi.