Desturi za kitamaduni na ukosefu wa uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake zimetambuliwa kama sababu kuu za dhulma za kijinsia katika Kaunti ya Lamu. Wadau wanasema licha ya kampeni za uhamasisho zinazoongozwa na serikali, mila za tangu jadi zinaendelea kuwa kichocheo cha utekelkezaji wa dhulma hizo.Wakizungumza wakati wa kikao cha wadau kilichoandaliwa kutathmini hatua zilizopigwa kupambana na dhulma za kijinsia na unyanyasaji wa watoto, washiriki walielezea wasiwasi kuwa waathiriwa wengi, hasa wanawake, bado wako katika mahusiano yanayoendeleza dhulma kutokana na utegemezi wa kifedha.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News