MISA yatoa mafunzo kukabiliana na habari potofu

  • | VOA Swahili
    14 views
    Kituo cha Radio Islam Mtangazaji wa Redio, Shakira Juma anasema anaziangalia taarifa zinazotumwa kwenye mitandao ya kijamii kwa mashaka. Shakira Juma, Mtangazaji wa Radio Islam: "Ninachagua kuhusu habari ambazo ninaziamini , au la, kwa sababu ya habari za uongo katika mitandao ya kijamii, machapisho bandia ambayo yanatokea siku hizi. Hivyo ndivyo hali ilivyo. Siwezi kuamini chochote." Wasemavyo Wakufunzi Wakufunzi wanasema habari za uongo zimekithiri nchini Malawi kwa kiasi kikubwa kutokana na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanakimbilia kuwatapeli waandishi wa habari kwa kuchapisha habari ambazo hazijathibitishwa, za udanganyifu, au hata kuvumbuliwa. Chisomo Kachapila anatoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuangalia taarifa za ukweli nchini Malawi. Nchini Malawi ambako kuthibitisha habari sahihi kumejaa changamoto, Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika MISA inafanya kazi ili kuboresha usahihi wa kuripoti na kuwasaidia waandishi wa habari kujenga uaminifu. Chisomo Kachapila, Mkufunzi wa Ukaguzi kujua Habari za Ukweli:"Kwa sababu pia wakati mwingine kama vyombo vya habari, tumeangukia katika mtego huu, ambapo taarifa tunazosema ni za wale ambao wako katika uongozi. Hatuzungumzii taarifa zinazowahusu watu. Kwa hivyo hivi sasa watu, watazamaji wamekuwa waandishi wa taarifa zao wenyewe. Kwa hivyo, shida iliyopo ni kwamba hawana ufahamu kuhusu vyombo vya habari. Tumeona picha walizopiga, picha za kutisha walizochapisha. Hawajui madhara yaliyopo katika maadili." Kachapila anasema kuwa kudukua habari za uongo imekuwa changamoto kwa sababu kuna taarifa chache sana kuhusu habari za ndani katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara. Chisomo Kachapila, Mkufunzi wa Ukaguzi unaoangazia Habari za ukweli anasema: "Kwa hivyo, kwa mfano, ukipiga picha ambayo ilichukuliwa katika ulimwengu wa Magharibi, utagundua kwamba ukienda na kuiangalia ili upate uthibitisho, ni rahisi kufanya hivyo. Tunahitaji taarifa zaidi zinazotuhusu sisi kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, kutoka Kusini mwa Afrika, kwenye mtandao, ili kurahisisha kazi hii. Vinginevyo, sio rahisi kufanya uchunguzi kujua ukweli wa taarifa katika muktadha wetu kama ilivyo katika ulimwengu wa Magharibi." ⁣ Ripoti ya Mwandishi wa VOA Lameck Masina kutoka Lilongwe, Malawi.⁣ ⁣ ⁣ ⁣ ⁣ #habaripotofu #malawi #lilongwe #waandishi #habari #MISA #kusinimwaafrika #usahihi #uaminifu #voa #voaswahili