Mji wa Freetown wabaki mtupu licha ya serikali kuondoa amri ya kutotoka nje

  • | VOA Swahili
    180 views
    Mji mkuu wa Sierra Leone Freetown unaonekana mtupu hii leo licha ya serikali kuondoa amri ya kutotoka nje iliyowekwa kufuatia shambulizi kwenye kambi ya kijeshi. Serikali ilisema kuwa vikosi vya usalama vimewakabili wanajeshi walioasi ambao walijaribu kuingia katika ghala la silaha jijini Freetown jana jumapili. Harrison Kamau ana taarifa zaidi #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.