MOROCCO YAFADHILI ELIMU MALINDI

  • | Citizen TV
    298 views

    Ubalozi wa Morocco nchini umetoa ufadhili wa shilingi milioni 12 kupiga jeki elimu hasa kwa vijana walioathirika na mihadarati katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi.

    Kwenye ziara katika shule ya jamii ya Town Secondary iliyopokezwa ufadhili huu, balozi wa Morocco Abderrazzak Laassel amesema wataendelea kuangazia shughuli zaidi za elimu ili kuhakikisha vijana zaidi wanapata elimu. Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Farid Sheikh alisema kuwa, kufikia Sasa, takriban vijana 50 wasiojiweza wamefaidika na ufadhili wa elimu.