Moto wa msituni wateketeza nyumba, maelfu ya watu watafutiwa hifadhi

  • | VOA Swahili
    82 views
    Wafanyakazi wa zima moto wameendelea kupambana na moto mkubwa kote kaskazini mashariki mwa Japan katika mji wa mwambao wa Ofunato Ijumaa (Februari 28). Kanda za video zilizochukuliwa kutoka angani zilionyesha moshi ukipaa angani kutoka upande wa eneo la msitu mlimani na mabaki ya majengo yaliyoteketea kwa moto. Moto huo unakadiriwa umeunguza kiasi cha hekta 1,200 (eka2,965), shirika la utangazaji la Japan NHK limeripoti Ijumaa, likiwanukuu maafisa wa eneo. Mtu mmoja amefariki. Zaidi ya kaya 1,300 katika eneo wamehamishwa ikiwa nimatokeo ya moto huo, vyombo vya habari vya eneo vimeripoti,huku watu zaidi ya 3,000 wakitafuta hifadhi katika maeneoyaliyotengwa kuwapokea. - Reuters #ofunato #japan #moto #wazimamoto #mlimani #japannhk #vifo #voa #voaswahili #motowamsituni