Wadau katika sekta ya maji wamezindua Mpango endelevu wa Utoaji Maji na Usafi wa Mazingira kwa Miji ya humu nchini, mradi unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi katika kaunti zote 47 nchini. Mpango huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo barani Afrika kwa ushirikiano na serikali ya Kenya huku ugavi wa fedha ukitengwa wa makundi matatu ya Rift Valley, Athi na Tana.
Akizungumza wakati wa warsha ya kuwahamasisha wanahabari kuhusu mradi huo jijini Nairobi, Mshirikishi kundi la Rift Valley linalojumuisha kaunti 23, Philip Kimeli, alisema kuwa zaidi ya miradi 15 ya usambazaji maji na ujenzi wa mifumo ya kuondoa majitaka, inatekelezwa katika maeneo hayo, ambapo asilimia 90 ya miradi hiyo imekamilika.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN
Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#KBCchannel1 #Kenya #News