Mruka parachuki anasa juu ya paa uwanjani

  • | BBC Swahili
    4,468 views
    Tazama namna mruka parachuti huyu alivyoachwa akining'inia kwenye paa la uwanja baada ya kunasa wakati wakishusha mpira kwa ajili ya kuanza kwa mechi ya mchezo wa raga. Wengine wawili waliokuwa wakiruka na parachuti kwa ajili ya kupeleka mpira wa mechi uwanjani walifanikiwa kutua salama katika uwanja wa Stade de Toulouse, kabla ya mechi ya Kombe la Mabingwa kati ya Sale na Toulouse, lakini mwenzao alipoteza mwelekeo na akabaki akining’inia kwenye paa baada ya kunasa juu. Mechi ilicheleweshwa kwa dakika 40 kabla ya kuanza. #bbcswahili #mechi #raga Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw