Mkuu wa mawaziri na waziri wa mashauri ya kigeni Musalia Mudavadi sasa anawataka wakenya kukoma kuingilia siasa au kupigania haki za mataifa mengine. Akirejelea visa vya wakenya waliotekwa nyara na kuzuiliwa karibuni mataifa ya Uganda na Tanzania, Mudavadi amesema hakuna uhakika wa uhuru uliopo Kenya kwenye mataifa hayo. Aidha amewataka vijana kutotumia vibaya mitandao ya kijamii anayosema inachunguzwa pakubwa na mataifa ya kigeni. Alikuwa akizungumza alipofungua kongamano kuhusu akili unde katika chuo kikuu cha Moi, mjini Eldoret