Mustakabali wa KBC : Serikali yajitolea kuboresha muundombinu

  • | KBC Video
    18 views

    Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi dijitali William Kabogo ametoa hakikisho kwamba serikali itaboresha muundo mbinu wa shirika la Utangazaji humu nchini, KBC ili kuliwezesha kutekeleza majukumu yake. Akiongea alipoongoza ujumbe wa ubalozi wa Romania humu nchini kwa ziara ya jumba la Broadcasting jijini Nairobi Kabogo aligusia nia ya serikali ya kubuni ubia na wadau mbalimbali kwa lengo la kuweka huduma za shirika hili kwenye mifumo ya kidijitali. Balozi wa Romania humu nchini Gentiana Serbu alieleza kuridhishwa na kujitolea kwa Kenya kubuni ubia na mataifa mengine katika sekta ya teknolojia.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News