muungano wa KMPDU watishia kugoma iwapo serikali haitafanikisha ahadi zake

  • | K24 Video
    4 views

    Zimesalia siku kumi na moja kwa serikali kufanikisha ahadi zake kwa wahudumu wa afya chini ya muungano wa KMPDU, la sivyo watasitisha huduma zao. Huu ndio msimamo katika awamu ya pili ya maandamano ya madaktari wanagenzi wa muungano huo ambao wamelalamikia ucheleweshaji wa mishahara yao kwa zaidi ya miezi minne. KMPDU sasa imetangaza kufanya maandamano ya kitaifa jumatatu wiki ijayo.