Mvuvi mwanamke Kenya

  • | BBC Swahili
    246 views
    Kutana na Pauline Mwaka, mwanamke mwenye umri wa miaka 28, anayekabiliana na changamoto ya mila ya zamani ya kuto mruhusu mwanamke kuingia kwenye uvuvi wa bahari kuu. Jamii yake ya pwani huko Kilifi, Kenya inaamini kuwa wanawake kujitosa majini huleta dalili mbaya na kusababisha ajali na masaibu kwa wavuvi wa kiume baharini. Lakini amedhamiria kwenda kinyume na dhana hiyo na ndiye mwanamke wa kwanza katika jamii yake kuthubutu. Anatumai safari yake haitabadilisha maisha yake tu bali pia itabadilisha maoni ya jamii yake kuhusu jukumu la wanawake. Katika mwaka ambao amekuwa akivua samaki, amewavutia wanawake wengine wawili kuungana naye baharini. ✍🏽: @ahmedbahajjofficial 🎥: @frankmavura Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw