Skip to main content
Skip to main content

Mwalimu mkuu wa shule ya Munyuki, Kakamega atoweka

  • | KBC Video
    3,161 views
    Duration: 1:56
    Familia ya mwalimu mkuu wa Shule ya mseto ya Sekondari ya Munyuki huko Lugari, Kaunti ya Kakamega, inahangaika kufuatia kutoweka kwa mwalimu huyo kwa njia isiyoeleweka. Simon Shange Isiaho anadaiwa kuondoka nyumbani kuelekea shuleni Jumatatu asubuhi, lakini hakufika shuleni.Mke wake, Salome Mukuna, anasema alifahamishwa kwamba gari la mwalimu huyo lilipatikana limeachwa karibu na kituo cha mabasi cha Lumakanda kando ya barabara ya Eldoret–Webuye, baada ya kuhusika katika ajali ndogo. Familia yake imemtafuta kwenye hospitali na vyumba vya kuhifadhi maiti bila mafanikio, huku polisi wakianzisha uchunguzi wa tukio hilo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News