Mwanafunzi asema alipata hasara na aibu baada ya kusambaza uzushi

  • | VOA Swahili
    578 views
    Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mwanafunzi wa chuo kikuu Portia Fafali Gedza anatambua vyema kuhusu athari ya habari za uongo kwenye WhatsApp kuhusu Makamu wa Rais wa Ghana Mahamadu Bawumia kwamba alikuwa anatoa pesa taslimu. Portia Fafali Gedza, mwanafunzi wa chuo kikuu anasema: “Mtu mmoja alinitumia kiungo cha taarifa kwamba Bawumia anagawa pesa. Nilibofya tu kwenye kiungo hicho, nikapitia mchakato wote, na ilifika mahali ambapo ilibidi nisambaze habari hiyo kwenye WhatsApp. Niliisambaza, na mwisho wa siku, sikutapa pesa. Kuna mtu alikuja kuniambia kwamba hizi habari ni za uongo, kwa hiyo nisingewaamini. Kwa sababu fikiria muda nilitumia kusambaza viungo hivyo, sikuweza kufanya chochote, na hivo, nilikuwa natumia bundle zangu, nilikuwa nasambaza kitu ambacho ni uzushi. Nilipata aibu.” Ripoti ya Isaac Kaledzi, VOA, Accra, Ghana.⁣ #ghana #voa #uchunguzi #uhakiki #habaripotofu #accra #waandishi #mwanafunzi #chuokikuu