Mwanzilishi wa taulo za kike mbadala

  • | BBC Swahili
    280 views
    Idda Mihindi ni daktari wa tiba kwa binadamu na mbunifu wa afya katika sekta ya afya nchini Tanzania. Pia ni mwanzilishi wa kiwanda kinachozalisha taulo za kike mbadala (SODO) zinazoweza kutumika tena ambazo ni rafiki wa mazingira yaani ‘Fursa pads’. Kupitia ubunifu wake, Idda anachangia kufikia lengo la kupunguza changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya hedhi barani Afrika na kwingineko. Kupitia kipindi cha Waridi wa BBC Idda Mihindi anaanza kwa kumuelezea Esther Namuhisa teknolojia anayoitumia kutengeneza taulo hizo za kike mbadala nchini Tanzania. 🎥: @frankmavura #bbcswahili #waridiwabbc #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw