Nakhumicha amwondolea lawama Gachagua kwenye sakata ya vyandarua vya mbu

  • | Citizen TV
    7,053 views

    Aliyekuwa waziri wa afya Susan Nakhumicha amemwondolea lawama aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua kwenye sakata ya ununuzi wa vyandarua vya mbu, akisema gachagua hakuchochea kwa namna yoyote utoaji wa zabuni hiyo ya shilingi bilioni 3.7. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge ya masuala ya kigeni kupigwa msasa kuhusu nafasi ya mwakilishi wa kenya katika shirika la un habitat Nairobi, Nakhumicha alieleza kwamba taifa lilipoteza mamilioni ya fedha baada ya sakata hiyo kulipuka.