Narc Kenya yaandika barua kujitoa kutoka Azimio

  • | Citizen TV
    12,506 views

    Chama cha Narc Kenya kinachoongozwa na Martha Karua sasa kimetangaza nia yake ya kujitoa kutoka kwenye muungano wa Azimio. Kwenye barua yake, Narc Kenya kinasema kuwa, hakina nia ya kuendelea kusalia kwenye muungano huo, baada ya baadhi ya wanachama wake kujiunga na baraza la mawaziri. Haya yamejiri huku tofauti na mkanganyiko ukiendelea ndani ya chama cha Azimio kufuatia uteuzi wa wanachama wake wanne kuwa mawaziri.