Muungano wa Makanisa Nchini NCCK, umeomba Serikali na Mashirika ya kijamii kuangazia kwa kina visa vya Mimba za utotoni, Dhuluma za kijinsia, na Magonjwa ya Ukimwi na Saratani yanayoongezeka katika Kaunti ya Meru.
Wakizungumza Mjini Meru, viongozi wa NCCK ukanda wa Mashariki ya Juu wametamaushwa na hali hiyo inayohatarisha afya ya wakazi wa kaunti ya Meru.
Meru ni Miongoni mwa kaunti zinazoongoza kwa Mimba za utotoni, magonjwa ya Saratani, Maambukizi Mapya ya HIV kwa Vijana na dhuluma za kijinsia, huku idadi ya watu wenye msongo wa mawazo ikiendelea kuongezeka.