Ndoto ya Junior Starlets yazimwa

  • | Citizen TV
    448 views

    Ndoto ya timu ya Junior Starlets ya kufuzu katika michuano ya kombe la dunia kwa mwaka wa pili mfululizo, ilizimwa baada ya kufungwa mabao matatu kwa moja na timu ya cameroon. Wasichana hawa wasiozidi umri wa miaka 17 walibanduliwa kwa jumla ya mabao 4 kwa moja kwani kwenye mechi ya mkondo wa kwanza hapa jijini nairobi starlets ilipoteza kwa bao moja kwa bila. Wasichana hawa walio chini ya ukufunzi wa kocha mildred cheche walipania kushiriki michuano hii kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushiriki makala ya mwaka jana nchini Dominica.