Nini kilitokea katika mkutano wa Rais Trump na Zelenskyy?

  • | VOA Swahili
    113 views
    Mwandishi wa Habari wa VOA Misha Komadovsky alirekodi malumbano makali kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakiwa Ofisi ya Oval, White House Februari 28, 2025. Mkutano wa White House kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ulikuwa na lengo la kufikia makubaliano ya kuiruhusu Marekani fursa ya kupata madini adimu na uligeuka malumbano makali kati ya viongozi hao na Trump alimueleza Zelenskyy, “ Ama utafikia makubaliano au sisi tunajitoa.” Katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii baada ya mkutano huo, Trump aliashiria kuwa pendekezo la makubaliano limevunjika. “Nimegundua kuwa Rais Zelenskyy hayuko tayari kwa amani iwapo Marekani itahusishwa kwa sababu anahisi ushiriki wetu unampa fursa kubwa katika mashauriano,” Trump aliandika. Kufuatia ziara hiyo, Zelenskyy alibandika katika mtandao wa X: “Ahsante Marekani, nashukuru kwa msaada wenu, ahsante kwa ziara hii. Ahsante @POTUS. Bunge la Marekani, na watu wa Marekani. Ukraine inahitaji amani ya kudumu, na sisi tunalihangaikia hilo.” #trump #zelenskyy #ukraine #russia #voa