Ongezeko la mihadarati katika vyuo vikuu

  • | K24 Video
    6 views

    Mamlaka ya kupambana na mihadaratI, NACADA, imebaini kuwa ongezeko la utumizi wa mihadarati miongoni mwa wanafunzi wa elimu ya juu linahusishwa na maandamano ya mwaka jana yaliyoongozwa na Gen Z. Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurugenzi mtendaji wa nacada, anthony omerikwa, amesema kuwa vijana wengi waliokuwa wakishiriki maandamano walitumia mihadarati kwa madai ya uongo kuwa yanapunguza athari za vitoa machozi. NACADA imetoa orodha ya marafiki wa uovu huo na wahadhiri ni washukiwa wakuu wanaosambaza mihadarati vyuoni.