Panzi Tanzania: Wadudu wa kipekee wanaopatikana misitu wa Pugu

  • | BBC Swahili
    461 views
    Panzi Tanzania ni panzi wa kipekee anayepatikana kwenye misitu wa mazingira asili wa Pugu Kazimzubwi uliopo mkoa wa Pwani nchini Tanzania, Panzi huyu amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na rangi zake asilia zenye kufanana za zile za bendera ya Tanzania hivyo kuvuta hisia za wengi wakitaka kujua imewezekanaje. Msitu huu uliopo umbali wa kilomita 20 kutoka katika Jiji la Dar es Salaam pia unafahamika kwa jina la utani kama mapafu ya jiji la Dar es salaam kutokana na kuwa chanza muhimu cha hewa safi ya oksijeni kwa jiji hilo lenye watu takribani milioni saba Mwandishi wa BBC Eagan Salla alitembelea msitu wa Pugu Kazimzumbwi na kuandaa taarifa ifuatayo. #bbcswahili #tanzania #asili Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw