Polisi-5 washtakiwa kwa kuwasaidia washukiwa kutoroka

  • | KBC Video
    60 views

    Idara ya upelelezi wa masuala ya Jinai itafahamu kesho iwapo itapewa siku 14 kuwazuilia maafisa watano wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Gigiri ambao wanasemekana kuhusika na kutoroka kwa wafungwa 13 kutoka kituo hicho. Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ilimweleza hakimu anayesimamia kesi hiyo, Martha Nanzushi kwamba uchunguzi umeanza kubaini ikiwa maafisa hao walisaidia katika kutoroka huko ambapo mshukiwa wa mauaji ya wanawake 42 huko Kware, Collins Jumaisi alikuwa miongoni mwa waliotoroka.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive