Radio Citizen yashirikiana na hospitali ya St.Peter's Kawangware

  • | Citizen TV
    98 views

    Hospitali ya St. Peter's ambayo pia inamiliki chuo cha mafunzo ya utabibu imeshirikiana na Radio Citizen Kutoa huduma za matibabu bila malipo kwa Wakazi wa Kawangware kaunti ya nairobi. Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika uwanja wa DO Grounds, Muuguzi Kwamboka kutoka St. Peter’s alielezea furaha yake kwa mafanikio ya hafla hiyo, kwa kufaa jamii. Huduma zilizotolewa ni pamoja na ushauri wa matibabu, matibabu ya meno, huduma za macho, na utoaji wa dawa bure kutoka hospitali ya St. Peter’s.