Raila ataka mgao wa kaunti uongezwe hadi Ksh.450B

  • | Citizen TV
    1,986 views

    Kinara wa ODM Raila Odinga ametaka serikali za kaunti kuongezwa mgao hadi shilingi bilioni 450. Akizungumza huko Mombasa katika hafla ya Eid baraza, Odinga ameisuta serikali kwa kile alichodai ni kutelekeza majukumu ya kaunti. Kiongozi wa wachache bunge la kitaifa Junet Mohammed naye amemtaka aliyekuwa waziri Justin Muturi kufafanua ni vipi bunge lilitumia shilingi bilioni 27 badala ya bilioni 6 kwa ujenzi wa jumba la bunge.