Rais Ruto akamilisha ziara ya siku tano Mlima Kenya

  • | Citizen TV
    9,358 views

    Rais William Ruto amewataka wapinzani wake wa kisiasa kumpa nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa wakenya akisema siasa za mapema zitahujumu utendakazi. Akizungumza katika kaunti za nyeri na kiambu, rais ruto amesema yuko tayari kusalimu amri mwaka wa 2027 iwapo wakenya wataamua kumpumzisha. Kwa sasa anasema yuko mbioni kuhakikisha kuwa amewashawishi wakenya kumchagua tena kutokana na rekodi yake ya maendeleo.