Rais Ruto ataka kikosi cha usalama Haiti kisaidiwe

  • | KBC Video
    104 views

    Rais William Ruto ameisihi jamii ya kimataifa itoe rasilmali zinazohitajika kwa kikosi cha usalama nchini Haiti kinachoongozwa na Kenya. Rais amesema msaada huo unaojumuisha wafanyikazi, vifaa na mipangilio, utafanikisha uafikiaji wa lengo la kikosi hicho katika udumishaji wa usalama nchini Haiti. Aliongea jana jijini Port-au-Prince alikokutana na maafisa wa polisi wanaohusika katika mchakato huo. Kiongozi wa taifa anatarajiwa kuhudhuria kongamano la 79 la baraza kuu la Umoja wa Mataifa litakaloanza wiki ijayo jijini New York, Marekani.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive