Rais Ruto atetea ushirika na Raila Odinga

  • | Citizen TV
    3,355 views

    Rais William Ruto ametetea ushirika wa kisiasa na kinara wa ODM Raila Odinga akisema hatua hiyo inalenga kuwafaidi wananchi na kuleta umoja wa kitaifa. Akizungumza kwenye mazishi ya Seneta wa Baringo William Cheptumo, Rais Ruto amesema kuwa manifesto za Kenya Kwanza na ODM zinawiana, haswa kuhusiana na mipango ya nyumba na afya na hivyo umoja wao utakuwa na manufaa.