Rais Ruto: Msiwachoche vijana kuzua vurugu

  • | K24 Video
    1,136 views

    Rais William Ruto amewataka viongozi wa kisiasa kuepuka kuwachochea vijana na badala yake kuwatia moyo na kuwaongoza ili wapate ajira na kushiriki katika fursa za kibiashara. Rais alizungumza haya katika eneo la Cheptais, kaunti ya Bungoma, wakati wa ibada ya maombi iliyojumuisha madhehebu mbalimbali, ambapo pia alijiunga na viongozi wengine wa eneo hilo. Alisisitiza lengo la serikali yake kutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo hilo.