Rais Trump akutana na Mfalme wa Jordan White kwa mashauri ya kidiplomasia

  • | VOA Swahili
    63 views
    Rais wa Marekani Donald Trump Jumanne alimpokea Mfalme wa Jordan Abdullah II White House kwa mazungumzo ya kidiplomasia. Viongozi hawa wawili walizungumzia masuala ya kieneo, ikiwemo mustakbali wa Gaza, ambayo imekabiliwa na mashambulizi ya angani ya Israeli wakati mgogoro wa wanamgambo wa Hamas ukiendelea. Mkutano huo umefanyika muda mfupi baada ya Rais Trump kuonya kuwa "balaa kubwa itaanza" endapo Hamas, kikundi kilichopo katika orodha ya ugaidi, hakitawaachia mateka waliobakia ifikapo Jumamosi mchana. #trump #jordan #gaza #kingabdullah #voa