Rais Trump asema anaona 'Marekani itaimiliki kwa muda mrefu' Gaza

  • | VOA Swahili
    214 views
    Rais Donald Trump wa Marekani amesema anataka Marekani ichukue umiliki wa Gaza ikiwa ni msimamo baada ya taarifa zake za awali za kuwalazimisha wakazi wa Gaza kuhamishiwa nchi jirani za Jordan na Misri. Trump alitoa tangazo hilo la kushangaza Jumanne jioni baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu huko White House. Wakati maelfu ya wakazi wa Gaza wakirudi katika nyumba zao zilizobomolewa kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano la Januari 19 kati ya Israel na Hamas, Rais Trump siku ya Jumanne alitoa tangazo la kushangaza. Donald Trump, Rais wa Marekani: "Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza na tutaifanyia kazi." Matamshi hayo ya Trump yanavuka yale aliyosema mwezi uliyopita kwamba atawahamisha wakazi wa Gaza hadi nchi jirani za Jordan na Misri. Anasema anataka kujenga eneo hilo kuwa alichokiita “mandhari ya Kitalii ya Riviera katika Mashariki ya Kati. Ismael Mohammed, miaka 47, na familia yake, waliokoseshwa makazi upande wa kusini mwa Gaza wakiwa njiani kurejea katika nyumba zao zilizoharibiwa kabisa wakati ambapo sitisho la mapigano kati ya Hamas na Israel likiendelea, huko Gaza City, Januari 28, 2025. Ismael Mohammed, miaka 47, na familia yake, waliokoseshwa makazi upande wa kusini mwa Gaza wakiwa njiani kurejea katika nyumba zao zilizoharibiwa kabisa wakati ambapo sitisho la mapigano kati ya Hamas na Israel likiendelea, huko Gaza City, Januari 28, 2025. Donald Trump, Rais wa Marekani kila mtu niliyezungumza naye amelipenda wazo la Marekani kumiliki eneo hilo, kulijenga na kubuni maelfu ya nafasi za ajira, na kulibadili kuwa la kuvutia ambalo hakuna atakayelitambua. Hakuna mtu anayetaka kuliangalia kwasababu wanachoona ni vifo na uharibifu na vifusi. Trump alitoa tangazo hilo baada ya kumkaribisha Waziri mkuu wa Israel Benjamina Netanyahu huko White House. Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel: "Nimesema hili hapo kabla. Ninasema tena Wewe ndiye rafiki mkubwa wa Israel kuwahi kuwepo hapa White House." Trump hakufafanua jinsi anavyopanga kuchukua udhibiti wa Gaza eneo ambalo limeharibiwa na miezi 15 ya vita. Hakufuta uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Marekani. Haiko bayana kuikalia Gaza kutaingiliana vipi na lengo la Trump mwenyewe la kupanua mkataba wa Abraham kuihusisha Riyadh. Mkataba ambao aliousimamia ambao ulianzisha uhusiano kati ya Israel na nchi za Kiarabu mwaka 2020. - VOA, AP #trump #netanyahu #israel #gaza #us #voa