Rais wa China Xi akilakiwa na Rais wa Brazil Lula

  • | VOA Swahili
    180 views
    Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amempokea Rais wa China Xi Jinping alipowasili katika jumba la makumbusho la Modern Art Museum mjini Rio de Janeiro kuhudhuria Mkutano wa G20 Jumatatu (Novemba 18). Mazungumzo ya Viongozi wa G20 kuhusu biashara, mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa kimataifa yatafanyika huku kukiwa na mabadiliko makubwa ya sera za Marekani ambayo Trump ameapa kuyatekeleza atakapoingia White House Januari, kuanzia ushuru hadi ahadi ya mashauriano ya kupata suluhu ya vita vya Ukraine. Rais wa China Xi atakuwa na jukumu muhimu katika mkutano wa G20 uliogawanyika na mivutano ya siasa za kikanda katikati ya vita vinavyoendelea huko Gaza na Ukraine. ⁣ #rais #brazil #luladasilva #joebiden #xijinping #china #makumbusho #riodejaneiro #g20 #viongozi #marekani