- 14,050 viewsDuration: 3:48Rais Yoweri Museveni wa Uganda amethibitisha kuwa serikali yake iliwateka nyara wanaharakati wa Kenya Bob Njagi na Nicholas Oyoo akiwataja kuwa wataalam wa maandamano waliofanya kazi kwa karibu na mpinzani wake Bobi Wine. Katika mahojiano yaliyopeperushwa na kituo cha UBC, Uganda, Rais Museveni alikiri kupokea simu kutoka kwa viongozi wa Kenya walioshinikiza kuachiliwa kwa wawili hao. Pia alikiri kutumia utekaji nyara kama njia ya kuwakabili mahasidi wake wa kisiasa akidai wanatumiwa kuharibu taifa hilo