Rais wa zamani Obama azungumzia changamoto zilizopo katika uchaguzi 2024

  • | VOA Swahili
    0 views
    Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama Jumanne aliwatahadharisha Wademokratik kuwa licha ya kuwa “uongozi umekabidhiwa “ kwa Harris, jukumu la Wademokratik bado halijamalizika. Obama alikuwa mzungumzaji mkuu katika usiku wa pili wa mkutano wa chama huko Chicago. Alitahadharisha dhidi ya kuridhika na hali hii wakati wa uchaguzi wa Novemba na kuwahimiza Wamarekani kupiga kura. “Msifanye kosa, itakuwa ni mapambano,” Obama alisema. Kwa nguvu zote za ajabu tulizoweza kuzikusanya, Kwa mikutano na ushawishi uliotapakaa, “Huu bado utakuwa uchaguzi wenye ushindani katika nchi iliyo na mgawanyiko.” - AP #dnc #obama #harris #voa