Ripoti ya Michezo ya Brookside Shule za Upili, Muhula wa Kwanza

  • | K24 Video
    20 views

    Ijapokuwa wamezimwa katika mashindano ya kitaifa ya uigizaji huko Nakuru, mabingwa watetezi wa mpira wa kikapu Butere girls wako katika fainali. Butere girls itapambana na kaya tiwi katika fainali ya michezo ya brookside ya shule za upili muhula wa kwaza hapo kesho katika kaunti ya Mombasa. Katika fainali zengine, Vihiga boys itamenyana na Kisii katika mchezo wa raga ya wachezaji 15 kila upande nao vigogo wa mpira wa magongo St Joseph girls Kitale watachuana na Tigoni.