Ruto aongoza taifa kumuomboleza aliyekuwa mchezaji wa Malkia Strikers Janet Wanja

  • | Citizen TV
    1,343 views

    Rais William Ruto ameongoza taifa kumuomboleza aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya voliboli malkia strikers janet wanja, aliyefariki jana usiku baada ya kuugua ugonjwa wa saratani kwa muda mfupi. Katika ujumbe wake wa rambirambi, Rais Ruto alisema Wanja alikuwa nyota mwenye kipaji na nidhamu ambaye aliitumikia Kenya kwa kujitolea na heshima katika mchezo wa voliboli. Katibu wa wizara ya Michezo Peter Tum akimkumbuka Wanja kutokana na michezo ya Olimpiki ya Paris akisema alikuwa mtu wa kujitolea, kocha mzuri na rafiki wa wengi. Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga pia ni miongoni mwa manahodha wengi ambao wamejiunga na mashirikisho yao kutuma ujumbe wa rambirambi.