Serikali inalenga kushirikiana na bara Ulaya kuwekeza katika uchumi wa baharini

  • | Citizen TV
    578 views

    Serikali inalenga kushirikiana na umoja wa bara ulaya ili kutafuta wawekezaji wa kibinafsi katika sekta ya uchumi wa bahari na maswala ya uvuvi. Waziri wa madini na uchumi wa bahari Salim Mvurya amesema kuwa wawekezaji hao watajumuishwa kwenye miradi tofauti ya serikali inayotekelezwa katika eneo la Pwani. Akizungumza katika kongamano la pili la Blue Invest Africa linalofanyika huko Diani kaunti ya Kwale, Mvurya amesema ushirikiano wa Kenya na mataifa ya EU katika uwekezaji wa miradi hiyo utaboresha uchumi wa taifa akisema serikali imewekeza zaidi ya bilioni 20 katika sekta hiyo.