Serikali kesho itaanzisha rasmi usajili wa bima ya Social Health Authority

  • | Citizen TV
    228 views

    Huduma za afya ya umma kuanzia hapo kesho zitatolewa kupitia bima mpya ya afya ya SHA. Hii ikimaanisha kuwa utumizi wa Bima ya NHIF iliyokuwa ikitumika umesitishwa. Haya yanajiri huku Kamati ya bunge kuhusu afya iliyokuwa na tashwishi kuhusiana na bima hii hapo awali ikiidhinisha utekelezwaji wake baada ya kupata majibu kuhusiana na maswali yote yaliyoibuka kuhusu mradi wa mfumo wa dijitali wa mpango huu.