Serikali kuu yashutumiwa kwa kutounga mkono ugatuzi

  • | Citizen TV
    491 views

    Baraza la Magavana limetishia kusimamisha utoaji huduma katika kaunti zote 47 katika siku 14 zijazo iwapo serikali haitaangazia malalamishi kuhusu kukatwa kwa bajeti ya kaunti kwa takriban shilingi bilioni 38. Kulingana na magavana, sehemu ya fedha hizo ni ruzuku kutoka kwa wafadhili ambayo ilikuwa imetengewa miradi mbalimbali lakini ilielekezwa kwingine wakati wa kupitishwa kwa Mswada wa Fedha za Ziada kwa Serikali za Kaunti.