Serikali ya Kwale yatoa ksh. 95.6m kwa wanafunzi 2,700

  • | Citizen TV
    398 views

    wanafunzi zaidi ya 2,700 wa shule za sekondari katika kaunti ya Kwale wamepokezwa fedha za basari za muhula wa kwanza . Serikali ya kaunti ya Kwale imetoa fedha hizo takriban shilingi milioni 95.6 kufadhili masomo ya wanafunzi wa shule za kitaifa kupitia mpango wa Elimu Ni Sasa. Akizungumza wakati wa kutoa hundi hiyo, gavana wa Kwale Fatuma Achani amewataka wanafunzi wanaofadhiliwa kuhakikisha wanafanya vyema kwenye mitihani yao ili kuepuka kuondolewa kwenye mpango huo wa basari.