Skip to main content
Skip to main content

Serikali yachukua hatua kushughulikia uhaba wa maji

  • | KBC Video
    71 views
    Duration: 2:11
    Serikali ya taifa imechukua hatua kusuluhisha tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji katika kaunti ya Kilifi kufuatia malalamishi ya wakazi na wawekezaji wa sekta ya utalii. Waziri wa maji, Eric Muga, aliongoza ujumbe wa maafisa wa serikali waliozuru kaunti hiyo ambao walibaini kwamba mtambo muhimu wa usambazaji maji umeharibika.Kaunti ya Kilifi imekuwa ikikumbwa na uhaba mkubwa wa maji huku kampuni za usambazaji maji za Kilifi Mariakani na ile ya Malindi zikishindwa kukidhi hitaji. Serikali imedhamiria kuweka mtambo unaotegemea kawi ya miale ya jua kusambaza maji katika eneo hilo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #KBCchannel1 #Kenya #News