Serikali yaendelea kuwajeresha wakenya waliokwama Myanmar

  • | Citizen TV
    652 views

    Serikali kupitia Ubalozi wa Kenya nchini Thailand inaendeleza zoezi la kuwarejesha nyumbani wakenya walilojikuta kwenye mtego wa ulaghai nchini Myanmar. Wakenya 78 waliwasili nchini hii leo, wiki mbili baada ya wengine 48 kurejea, walipongeza juhudi za serikali za kuwaokoa kutoka kwa mateso. Katibu katika wizara ya maswala ya kigeni Roseline Njogu, aliwaonya vijana dhidi ya kutumia maajenti wasiokuwa na leseni kutafuta kazi ughaibuni. Serfine Achieng Ouma ana maelezo zaidi.