Serikali yafunga kanisa la St. Joseph Messiah in Africa, Rongo

  • | Citizen TV
    260 views

    Kikosi cha wanasheria wa Kanisa la St Joseph Messiah in Africa kimetetea haki za waumini wao dhidi ya agizo la serikali la kulifunga kanisa hilo lenye utata huko Rongo, eneo la Opapo kaunti ya Migori. Uamuzi wa Naibu Kamisama wa Rongo George Matundura kuwazuia waumini wa dhehebu hilo kuingia ndani ya kanisa hilo na kuwalazimisha kurejea nyumbani umeibua hasira na wasiwasi kwa wawakilishi wa kisheria wa kanisa hilo......hatua hiyo ilichukuliwa baada ya watu wawili kufariki wakitafuta uponyaji katika kanisa hilo. Wakili wa kanisa hilo Benard Acholla amesema atawasilisha ombi mahakamani kupinga agizo la serikali.