Serikali yakusanya maoni kuhusu mabadiliko ya sera ya biashara ndogondogo, Nyeri

  • | Citizen TV
    84 views

    Uvumbuzi, Utafiti wa data kuhusu sera ya wafanyabiashara wadogo ni kati ya sera ambazo serikali inanuia kutekeleza, ili kuliziba pengo linalozuia kukua kwa biashara ndogo nchini. Serikali inaendeleza mchakato wa kubadilisha sheria ya mwaka 2020, inayozidhibiti biashara hizi. Haya ni kwa mujibu wa idara ya Biashara ndogo inayokusanya maoni kutoka kwa wakenya kuhusu kubadilishwa kwa sheria hiyo, baada ya kubainika kwamba asilimia 84 ya biashara ambazo huanzishwa nchini hufilisika kabla ya mwaka mmoja kuisha.