Shahidi wa mauaji ya mwandamanaji Rex Masai ajiondoa

  • | Citizen TV
    3,114 views

    Mmoja wa mashahidi wakuu katika kesi ya mauji ya mwandamanaji Rex Masai, amejiondoa kwa kuhofia usalama wake. Akizungumza na runinga ya Citizen mamake marehemu Rex Masai, alielezea wasiwasi alionao kuhusu hatma ya kesi ya mwanawe akidai kuwa huenda kuna njama ya kuficha ushahidi. Rais wa chama cha mawakili nchini LSK, Faith Odhiambo amemsuta mkuu wa mashtaka ya umma kwa kudai kuwa mashahidi hawajajitokeza akimtaka aweke mikakati ya kuwahakikishia usalama wao .